Serikali: Uwanja mpya wa Simba kupunguza mzigo Lupaso
DAR ES SALAAM — Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hamis Mwinjuma, amepongeza uamuzi wa Simba kujenga uwanja wa mashabiki 10,000 hadi 12,000, akisema utasaidia kwa michezo ya ndani na kupunguza mzigo kwa Uwanja wa Mkapa.
Ameahidi kuwa Serikali itaendelea kuwaunga mkono Simba katika safari yao ya kutafuta ubingwa wa Afrika.
Akizungumza katika hafla hiyo, Mwenyekiti wa Simba, Murtaza Mangungu, ameeleza kuwa mchakato wa tenda ulifanywa kwa uwazi na kushirikisha kamati za bodi.
Pia ameipongeza Jayrutty kwa kuibuka mshindi na kuahidi ushirikiano thabiti na mwekezaji Mohammed Dewji kuhakikisha utekelezaji wa miradi yote unafanikiwa.
PIA SOMA: Simba kujenga studio, uwanja na kuvaa jezi za kimataifa
“Mapinduzi makubwa ya jezi yalifanywa na Kassim Dewji kwa zaidi ya miaka 10. Miaka hiyo tulikuwa tunaletewa tu jezi nyeupe na nyekundu lakini yeye akaleta jambo la tofauti lakini game changer ni Vunja Bei yeye ndio akuja kuonyesha njia, Sandaland alifanya kazi yake lakini sasa amekuja Jayrutty.”- Mwenyekiti wa Klabu, Murtaza Mangungu
Mangungu pia ametambua mchango wa watu waliowahi kuleta mapinduzi kwenye uuzaji wa jezi, akiwemo Kassim Dewji, Vunja Bei na Sandaland, huku akisema Jayrutty sasa ndiye “game changer” mpya atakayobadilisha taswira ya klabu hiyo kitaifa na kimataifa.



