Serikali yaahidi kusimamia usalama wa afya

DODOMA: Waziri wa Afya, Jenista Mhagama, amesema kuwa serikali itaendelea kusimamia usalama wa afya za Watanzania kwa kufuata miongozo ya usimamizi wa afya nchini.
Akizungumza na vyombo vya habari kuhusu tamko la Rais wa Marekani, Donald Trump, la kusitisha misaada ya afya kwa nchi za Afrika, Waziri Mhagama alisema kuwa serikali imepokea tamko hilo na kwa sasa wapo katika mchakato wa kufuatilia zaidi ili kutoa taarifa kamili kwa umma.
Aidha, Waziri Mhagama amewataka Watanzania kuendelea kuwa watulivu katika kipindi hiki na kusema kuwa serikali itatoa taarifa rasmi kwa umma mara itakapokuwa na maelezo zaidi kuhusu suala hilo.
Hivi karibuni, Rais Trump alitangaza kusitisha misaada ya afya kwa nchi za Afrika, ikiwemo Tanzania, hususan usambazaji wa dawa za ARVs, hatua ambayo imezua taharuki miongoni mwa watanzania ambao wanategemea dawa hizo ili kurefusha maisha yao.
SOMA: Kituo cha afya cha mil 632/- chazinduliwa Babati



