Kituo cha afya cha mil 632/- chazinduliwa Babati

MANYARA: WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Profesa Kitila Mkumbo amezindua na kufungua rasmi Kituo cha Afya cha Bashnet kilichopo katika Kata ya Bashnet Halmsahauri ya Wilaya ya Babati Vijijini kinachotajwa kugharimu Sh milioni 632.

Uzinduzi wa kituo hicho umefanyika leo Januari 4, 2025 katika wilaya ya Babati Vijijini mkoani Manyara, ikiwa ni mwisho wa ziara yake ya siku tatu mkoani humo.

Prof Kitila amesema ni dhamira ya serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan kuimarisha huduma ya afya nchini na kuongeza vituo vya afya kila kata kwa lengo la kuhakikisha afya ya kila mtanzania inakuwa salama.

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na Mbunge wa Babati Vijijini, Danieli Sillo ameeleza jinsi gani kituo hicho kinavyoenda kuwa msaada kwa wakazi wa kata ya bashnet kwani jumla ya wakazi 17,725 watanufaika na kupatiwa huduma katika kituo hicho.

Akisoma taarifa fupi ya utekelezaji wa mradi huo kwa niaba ya kamati ya usimamizi wa kituo hicho, Dk Paschal Mao amesema jumla ya majengo manne(04) yamejengwa kwa awamu ambalo ni jengo la wagonjwa wa nje (OPD), maabara,jengo la wazazi (Martenity_combined) na jengo la kuhifadhia maiti (mortuary) ambayo yamekamilika kwa asilimia 100(%) na kuanza kutumika.

Habari Zifananazo

Back to top button