Serikali yabaini changamoto utitiri nyumba za ibada

DAR ES SALAAM: Serikali imesema imebaini kuwepo kwa changamoto ya uanzishwaji holela na utitiri wa nyumba za ibada katika maeneo mbalimbali hapa nchini.

Hayo yamesemwa leo Machi 26, 2024  na Waziri wa Mambo ya Ndani, Hammad Masauni katika uzinduzi wa Kampeni ya Usajili wa Jumuiya za Kiraia itakayofanyika nchi nzima.

Amesema baadhi ya jumuiya za dini hususan makanisa na misikiti imebainika kujengwa katikati ya makazi ya watu, kuna mrundikano wa taasisi nyingi kwenye eneo dogo na baadhi ya taasisi kutumia sauti za juu na hivyo kusababisha adha na usumbufu katika jamii.

“Tunafanya usajili wa jumuiya za kiraia ili zile zinazoenda kinyume na sheria tutazifuta,”amesema.

Amesema changamoto zote hizo zinahitaji ushirikiano wa pamoja katika ushughulikiwaji wake, ili kuendelea kudumisha hali ya utulivu na usalama katika maeneo ya wananchi.

Habari Zifananazo

Back to top button