Serikali yaeleza mpango kukabili majanga ya moto

DODOMA; SERIKALI imesema mpango wake ni kusambaza magari ya zimamoto na uokoaji kwa wilaya zote nchini kwa ajili ya kukabiliana na majanga ya moto.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Daniel Sillo ametoa kauli hiyo bungeni leo, alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Kyerwa, Innocent Bilakwate aliyetaka kujua lini serikali itapeleka gari la Polisi na gari la zimamoto katika wilaya ya Kyerwa ili kukabiliana na majanga ya moto.
“Serikali kupitia Jeshi la Polisi imepeleka gari jipya moja aina ya Toyota Land Cruiser Pickup kwa Polisi Wilaya ya Kyerwa.
“Aidha kwa upande wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Serikali itapeleka gari moja katika wilaya hiyo ikiwa ni mpango wa serikali wa kusambaza magari ya zimamoto na uokoaji kwa wilaya zote nchini kwa ajili ya kukabiliana na majanga ya moto.