SERIKALI imendelea kuwekeza zaidi katika sekta ya Tehama ilu kukuza zaidi sekta ya mawasiliano ikiwemo mifumo ya kidigitali katika kuhakikisha maendeleo ya kiuchumi na kijamii yanakua zaidi.
Aidha sayansi, teknolojia na ubunifu ni lazima vipewe msukumo ili kuongeza ufanisi na upatikanaji huduma kwa wananchi na kuagiza mikoa miwili ambayo hairs katika mfumo wa Ofisi Mtandao ijiunge ifikapo Juni 30 mwaka huu
Hayo yamesemwa na Makamu wa Rais, Philip Mpango kwaniaba ya Rais Samia Hassan Suluhu wakati wa ufunguzi wa mkutano wa 5 wa mwaka wa Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA) wenye kauli mbiu isemayo “Utekelezaji wa Jitihada za Serikali Mtandao na Ubunifu kwa utoaji wa huduma bora kwa umma” ikiwa na lengo la kuchochea ubunifu na utekelezaji wa jitihada za serikali mtandao kwa taasisi za umma, ili kuongeza ufanisi wa utendaji kazi na utoaji wa huduma bora kwa umma”
Amesema katika kuhakikisha sekta ya Tehama inaimarika zaidi Tehama ni vema ipewe mkazo ikiwemo kuandaa vijana wataalam katika sekta hiyo ili kukuza umahiri wa tafiti na ubunifu katika kufika malengo ya serikali mtandao
“Serikali itaendelea kuweka mazingira wezeshi ya ufundishaji vyuo vikuu na taasisi za serikali ili kuleta ukomavu katika utoaji wa huduma”
Ameagiza mikoa miwili isiyojiunga na e -Office ijiunge ifikapo Juni 30 mwaka huu na kuagiza vituo vya umahiri kupitia Tehama zipewe msukumo zaidi ikiwemo vipaumbele vya e-GA vifikiwe sanjari na mifumo kusomana ili kurahisisha utoaji huduma nzuri kwa wananchi