Serikali yafafanua utaratibu mgonjwa anayekosa dawa

DODOMA; Wizara ya Afya imevielekeza vituo vya kutolea huduma za afya kuweka utaratibu wa mgonjwa kupata dawa iliyokosekana hospitali aliyotibiwa, ili kuepusha usumbufu kwa wananchi.

Hatua hiyo imetokana na swali la Mbunge wa Nkenge, Larent Kyombo aliyehoji kuwaserikali haioni kufutwa kwa Form 2c katika huduma ya bima ya afya inakosesha mgonjwa kupata dawa iliyokosekana hospitali aliyotibiwa.

Akijibu swali hilo kwa niaba ya Waziri wa Afya, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Tamisemi), Festo Dugange amesema uamuzi wa kusitisha matumizi ya fomu za dawa (Form 2C) katika vituo vya kutolea huduma za afya ulifanyika kwa kuzingatia manufaa yake.

“Ikiwemo utekelezaji wa maelekezo ya watoa huduma wote wa serikali kuwa na utaratibu wa kuanzisha maduka ya dawa yanayomilikiwa na hospitali na hivyo kuongeza mapato ya ndani ya hospitali, kuepusha usumbufu kwa wananchi wa kutafuta dawa nje ya hospitali na hivyo kusabisha lawama zisizo za lazima kwa Serikali na kuepusha vitendo vya udanganyifu vinavyofanywa katika eneo la dawa dhidi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya.

“Hata hivyo, wizara imevielekeza vituo vya kutolea huduma kuweka utaratibu wa mgonjwa kupata dawa iliyokosekana hospitali aliyotibiwa ili kuepusha usumbufu kwa wananchi,” amesema.

Habari Zifananazo

Back to top button