Serikali yajizatiti kwenye mifumo ya Tehama

ARUSHA: SERIKALI inaendelea kuwekeza katika Tehama ikiwa ni njia mojawapo ya kuboresha Mkongo wa Taifa ili huduma za kidigital ziweze kupatikana kirahisi katika maeneo yote ya nchini ikiwemo huduma za kifedha.

Hayo yalisemwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, CPA Amos Makalla leo muda mfupi kabla ya kuzindua tawi jipya la Benki ya CRDB katika Mji wa Namanga wilayani Longido mkoani Arusha katika hafla iliyohudhuriwa na viongozi mbalimbali wa benki hiyo na serikali.

Makalla alisema Mkoa wa Arusha ni Mkoa wa Kitalii na kifugaji kwa asilimia mia hivyo huduma za kifedha kwa njia ya kidigital inahitajika sana ikiwa ni pamoja katika maeneo ya mipakani kutokana na hali hiyo ndio maana serikali imejikita katika kuboresha huduma ya Tehama katika maeneo yote ikiwa ni pamoja na kuhakikisha Mkongo wa Taifa unakwenda katika maeneo yote ya nchi.

Alisema uamuzi wa uongozi wa Benki ya CRDB kufungua tawi lake Namanga mpakani mwa Tanzania na nchi Jirani ya Kenya unapaswa kupongezwa sana kwani wafanyabiashara wa aina tofauti wa nchi hizo wakiwemo wafugaji watanufaika na huduma za kibenki kupitia benki hiyo.

Mkuu huyu wa Mkoa aliendelea kusema kuwa Mkoa wa Arusha ni Mkoa wa Kitalii na kifugaji na asilimia mia ya wageni wa kitalii ama wafugaji huwa hawatembei na fedha taslimu kwani hutegemea kufanya miamala ya kifedha kidigital na kwa sasa benki ya CRDB imekuwa mkombozi kwao.

Alisema na kuwahimiza wafugaji wakubwa kwa wadogo kuhakikisha wanafungua akaunti katika tawi la CRDB kwani hiyo ni moja ya fursa ya kijikwamua kiuchumi kwa kuweka fedha katika benki hiyo na kuwataka kamwe kuacha kutembea na fedha ntaslimu ama kuweka nyumbani kwani sio salama.

Makalla alisema kuanzishwa kwa Benki ya CRDB Namanga ni moja ya kiunganishi kikubwa kwa nchi ya Tanzania na nchi jirani ya Kenya na kuwataka wafanyabiashara wan chi hizo kutumia vema fursa hiyo katika kujikwamua kiuchumi.

Alisema fedha zina ibilisi mkubwa iwapo zitakuwa mfukoni ama nyumbani kwa kuwa na matumizi yasiyokuwa ya lazima lakini zikiwekwa benki matumizi yake yatakuwa ya Adamu na yenye msingi hivyo aliwaomba CRDB kuwekeza zaidi katika teknolojia mpya za kifedha lengo likiwa kuongeza ufanisi kwa wateja kuwafikia kwa urahisi mahali popote walipo.

Makalla alisema miaka 30 ya benki ya CRDB toka kuanzishwa kwake imeonyesha wazi ni jinsi gani ilivyoimarika katika kutoa huduma za kifedha na ameuka uongozi wa benki hiyo kutobweteka na kuendelea kubuni namna nyingine ya kidigital ili kuwafikia watanzania maeneo yote nchini.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa Wateja wadogo na Kati wa CRDB,Bonveture alisema kuwa Mkoa wa Arusha una matawi 15 pamoja na tawi la Namanga,mawakala 1,800 wakati Namanga kuna tawi moja na mawakala 120 na kutokana na hali hiyo wana uhakika wa utoaji huduma za kifedha katika Mji huo zitaimarika.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Longido Salimu Kally akiwakilishwa na Katibu Tawala wa wilaya hiyo,Rahma Kondo aliishukuru CRDB kwa uamuzi wake wa kufungua tawi katika Mji wa Namangan a kusema kuwa utaondoa usumbufu kwa wafanyabiasha Kwenda umbali mrefu kutafuta huduma ya benki hiyo.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button