Serikali yashauriwa mkakati maalum ukuzaji uchumi

MSHAURI Mikakati wa Shirika la Foundation for Civil Societies(FCS), Prudence Zoe Glorious ameshauri serikali kuwa kufikia mwaka 2050 ni muhimu kuwa na mkakati wenye lengo la Tanzania kuwa na uchumi wa kati ngazi ya juu.

Amesema uchumi huo utawezesha pato la mtanzania kuwa Dola 8000-12,000 huku Pato la Taifa likiwekwa malengo ya kufikia Dola Bilioni 700.

Hayo yameelezwa leo Dar es salaam katika Mkutano uliofanyika katima ya Asasi za Kiraia na timu Kuu ya Uandishi wa Rasimu ya Dira aya Taifa ya Maendeleo 20250 ili kucanya uhakiki wa rasimu ya kwanza ilitolewa Desemba 2024.

Aidha, Prudence ameshauri serikali pia kuweka mazingira bora ya kufanya biashara na kuvutia wawekezaji wa ndani na nje ya nchi, badala ya Rasimu ya kwanza ya dira 2050 ilivyo ambayo inavutia zaidi wawekezaji wa nje ya nchi badala ya kuzingatia na Wawekezaji wazawa wa ndani ya nchi.

Pia ameshauri serikali kuisaidia sekta binafsi kwa kuhakikisha kunakuwa na upatikanaji wa mitaji, masoko na mifumo imara ya kodi na shabaha ya tano ya Dira 2050 isomeke kuwa na sekta binafsi imara, huru na yenye ujasiri na uwezo wa kiushindani kwa kuwawekea mazingira bora ya upatikanaji wa mitaji na masoko ya uhakika.

Prudence amehimiza umuhimu wa uwajibikaji kwa watumishi wa umma utakaokuwa na tija na uwajibikaji kwa misingi ya weledi na uadilifu bila kufungamanishwa na mtu, mamlaka ama itikadi ya Chama fulani cha siasa

Wadau wa AZAKI wameshauri kuelekea 2050, Tanzania kuanza kuwa na mikakati madhubuti ya kuhakikisha tunaondokana na kuagiza bidhaa kutoka nje ya nchi na badala yake tuwe na mpango wa kuagiza bidhaa zetu wenyewe ili kukuza uchumi na kuongeza fursa za ajira kwa Vijana

Muwakilishi wa Shirila la Salama Foundation, Shadrack Msuya amesisitiza juu ya umuhimu wa kutumia Vyuo vya Veta katika kubuni na kutengeneza bidhaa mbalimbali ikiwemo Pikipiki badala ya kuishia kuwa mafundi wa bidhaa zinazoagizwa kutoka nje ya nchi.

Pia Msuya ameshauri kuelekea 2050 serikali ikaanzisha Makampuni ya Kimkakati kwenye malighafi zinazopatikana nchini ili kuwezesha mashirikiano ya kiumiliki kati ya Wazawa na wageni katika jitihada za kukuza uchumi na kuongeza mzunguko wa fedha kwa wananchi wa Tanzania.

Habari Zifananazo

Back to top button