Serikali yasisitiza ufanisi kwa Taasisi za Umma

SERIKALI imetoa onyo kwa taasisi na mashirika ya umma yasiyoonesha ufanisi, ikisema yako hatarini kufutwa au kuunganishwa iwapo hayatachukua hatua madhubuti za kuboresha utendaji wao.
Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam baada ya kikao cha ndani na menejimenti ya OMH kilichoongozwa na Msajili wa Hazina, Nehemiah Mchechu, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji Prof. Kitila Mkumbo amesema haiingii akilini kuona baadhi ya mashirika ya umma yakishindwa kutoa gawio stahiki licha ya uwekezaji mkubwa wa Serikali.

Aliongeza kuwa Serikali itatoa muda maalum kwa taasisi husika kujirekebisha kabla ya kuchukua uamuzi wa kuyaunganisha au kuyafuta pale itakapobidi. SOMA: “Mashirika ya umma yajifunze kwa binafsi”



