Serikali yazungumzia sanamu ya Nyerere

SERIKALI imetoa tamko rasmi kuhusu sanamu la hayati Mwalimu Julius Nyerere, iliyofunguliwa hivi karibuni Makao Makuu ya Umoja wa Afrika (AU) huko Addis Ababa, Ethiopia.

Balozi Said Shaib Mussa, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, ameeleza kwamba Serikali imepokea taarifa za kitaalamu kuhusu sanamu hiyo kutoka kwa kamati maalum.

Kamati hiyo ambayo ilijumuisha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo pamoja na mtoto wa Hayati Nyerere, Madaraka Nyerere.

Advertisement

Ilikubaliana kwamba sanamu hiyo inalingana kikamilifu na sura ya Hayati Nyerere kati ya miaka 1960 na 1980.

Balozi Mussa amebainisha kwamba kulingana na uchambuzi wa wataalamu, sanamu hiyo ina mfanano wa asilimia 92 na sura halisi ya Nyerere. Kwa mujibu wa vigezo vya kitaalamu, mfanano wa asilimia 75 unahitajika ili kuthibitisha kwamba sanamu inawakilisha mtu fulani kikamilifu.

Tamko hilo la Serikali limekuja wakati wa mkutano na wahariri wa vyombo vya habari Ikulu, Dar es Salaam, ambapo pia ilijadili kuhusu ziara ya Rais Samia Suluhu Hassan huko Vatican, Norway, na Addis Ababa, Ethiopia.