Serikali yazungumzia utekelezaji kiwanda cha saruji Kasulu

DODOMA; SERIKALI imesema kasi ya utekelezaji wa mradi wa kiwanda cha saruji cha Kasulu imekuwa ndogo, hivyo inataka utekelezaji wake uanze haraka iwezekanavyo.

Naibu Waziri wa Viwanda an Biashara, Dennis Londo ametoa kauli hiyo bungeni leo Februari 4, 2026, alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Kasulu Vijijini Edibily Kinyoma aliyehoji lini ujenzi wa Kiwanda cha Saruji (TACECO LTD) cha Kasulu utaanz,a ukizingatia mwekezaji alishapewa eneo miaka mitatu iliyopita.

“Ni kweli kuwa eneo lililopo katika kata ya Kagera Nkanda katika wilaya ya Kasulu lilitolewa kwa mwekezaji wa kampuni ya TACECO Ltd kutoka Burundi kujenga kiwanda cha saruji.

“Mwekezaji huyo yupo katika hatua ya kufanya tathmini ya kina (Feasibility Study) ya upatikanaji wa malighafi kama vile clinker, gypsum na Pozzolana. Hata hivyo, kasi yake imekuwa ndogo katika kutekeleza mradi huu.

Kwa sasa, Serikali inaendelea kumhimiza kuhakikisha kwamba mradi huu unaanza utekelezaji haraka iwezekanavyo,” amesema.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button