SGR yatengeneza ajira 9,376

DODOMA — Ajira za moja kwa moja 9,376 tayari zimezalishwa kupitia utekelezaji wa mradi wa reli ya kisasa ya SGR, huku kampuni 792 za Kitanzania zikihusishwa moja kwa moja katika kutoa huduma mbalimbali ndani ya mradi huo.
Akihutubia leo Juni 27, 2025 jijini Dodoma wakati wa kuhitimisha shughuli za Bunge la 12, Rais Samia Suluhu Hassan amesema kuwa hatua hiyo ni sehemu ya mafanikio makubwa ya serikali katika kuboresha miundombinu na kuinua uchumi wa ndani kupitia ushirikishwaji wa Watanzania.
Rais Samia pia ametangaza kuwa reli ya SGR imeanza rasmi kusafirisha mizigo kati ya Dar es Salaam na Dodoma, hatua itakayopunguza muda wa usafirishaji, kupunguza gharama, na kuimarisha nafasi ya Tanzania kama lango kuu la biashara kwa ukanda wa Afrika Mashariki.
“Kwa kuanza kwa safari hizi, tunachochea ukuaji wa biashara, tunarahisisha uunganishwaji wa masoko ya ndani na nje, na tunaipa Tanzania hadhi mpya ya kiuchumi barani Afrika,” amesema Rais Samia.
I am now making an extra $19k or more every month from home by doing a very simple and easy job online from home. sxs I have received exactly $20845 last month from this home job. Join now this job and start making extra cash online by following the instructions on the given website………………….. Www.JoinSalary.Com