Sh Bil 1.1  zanogesha ukarabati Mv Tanga

Zaidi ya Sh bil 1.1 zimetumika kufanya ukarabati wa kivuko cha Mv Tanga, ambacho kinatoa huduma ya usafiri eneo la Pangani – Bweni wilayani Pangani, mkoani Tanga.

Akizungumza katika hafla ya mapokezi ya  kivuko hicho, Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Omar Mgumba amesema  kivuko hicho kilianza kukarabatiwa Juni mwaka huu na hadi kufikia Oktoba ukarabati ulikuwa umemalizika.

Amesema kuwa kukamilika kwake kutasaidia kuboresha huduma za usafiri wa majini kwenye eneo hilo,  kwani sasa kutakuwa na vivuko viwili

“Niwaombe Shirika la Wakala wa  meli nchini (TASAC), kutekeleza jukumu la ukaguzi wa mara kwa mara ya vivuko nchini, ili kuhakikisha ubora na usalama wake,”amesema Mgumba.

Naye Mtendaji Mkuu wa TEMESA, Lazaro Kilahala, amesema kuwa katika mwaka huu wa fedha serikali inatarajia kutumia zaidi ya sh Bil 60.3Kwa ajili ya ujenzi wa vivuko vipya nane sambamba na ukarabati wa vilivyopo 14.

Habari Zifananazo

One Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button