Sh bilioni 5 kuendeleza ujenzi hospitali ya Rufaa Katavi

DODOMA: SERIKALI imetenga Sh bilioni 5 katika mwaka wa fedha 2023/2024 kuendelea na ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Katavi.

Kati ya fedha hizo Sh milioni 224.750 zimetengwa kwa ajili ya ujenzi wa jengo la huduma ya usafishaji damu.

Kauli hiyo imebainishwa na Naibu Waziri wa Afya, Dk Godwin Mollel leo bungeni jijini Dodoma wakati akijibu maswali kwa niaba ya Waziri Ummy Mwalimu.

Aidha, Dk Mollel amesema kuwa kwa mujibu wa tafiti zilizofanywa, matatizo yatokanayo na utoaji mimba ni moja ya sababu inayochangia vifo vitokanavyo na uzazi kwa asilimia 10%.

Hata hivyo,amesema madhara yanayotokana na utoaji wa mimba usio salama ni pamoja na uambukizo mkali wa mfumo wa uzazi (Septic Abortion) ambao unaweza kupelekea mgonjwa kutolewa mfuko wa uzazi na wakati mwingine kupoteza maisha.

Habari Zifananazo

Back to top button