Sh bilioni 755 zatekeleza miradi Kilimanjaro
MKUU wa Mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin babu amesema serikali imetoa zaidi ya Sh bilioni 755 katika kipindi cha miaka miwili na nusu fedha zilizotumika kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo mkoani humo.
Kiongozi huyo amesema hayo alipoongoza harambee ya kuchangia mwendelezo wa ujenzi wa ofisi za makao makuu ya Waadventista Wasabato jimbo la Kaskazini Mashariki mwa Tanzania katika Wilaya ya Kilimanjaro.
Amewaasa waumini na viongozi wa dini hiyo kuendelea kumuunga ,kono na kumuombea Rais wa Samia Suluhu Hassani kwa kazi kubwa anayoifanya kuleta maendeleo.
“Sh bilioni 755 zimetumika ikiwemo jengo la mionzi Hospital ya KCMC kuboresha huduma ya afya pia jengo la mama na mtoto katika hospitali ya mawezi pia manunuzi ya vifaa tiba,mradi mkubwa wa maji Same, Mwanga -Korogwe, Hospitali kubwa ya Wilaya ya Same lengo la Mhe.Rais ni kuona Wananchi wake wananufaika na huduma pia kupiga hatua kimaendeleo”. Alisema Nurdin Babu.
Aidha mkuu huyo wa mkoa amechangia Sh million 5 na kuwaasa wadau wengine kuunga mkono zoezi hilo .
Awali Mkuu wa Wilaya ya Same, Kasilda Mgeni alipongeza ushirikiano uliopo baina yao viongozi wa dini kwa serikali akisema imerahisisha utekelezaji wa shughuli mbalimbali ikiwemo mipango ya maendeleo kwenye wilaya hiyo.
“Nisisitize tuendelee kushikamana kutunza amani na upendo tunu ya taifa letu tangu enzi za waasisi wetu, niwaombe pia waumini na viongozi wa dini kuendelea kumuombea Mhe.Rais Dk Samia Suluhu Hassani aweze kuifanya vizuri zaidi kazi kubwa ya kujenga Taifa letu”. Alisema.
Askofu wa kanisani la Waadventista Wasabato Kaskazini Mashariki mwa Tanzania, Mussa Mzumbi amesema harambee ya ujenzi wa ofisi za Konferensi ni kwa yoyote atakayekuswa kuchangia kwa sababu ni sehemu ya ibada kwa Mungu na kujenga mahusiano mazuri kwa Watanzania na ambao sio Watanzania.
“Tulipoanza hadi kufikia hatua hii zimetumika Sh milion 416,484,000 na changizo hili la kuchangia zaidi ya Sh milioni 685 ni kwa ajili ya kuendeleza tunategemea kukamilisha eneo la chini na kupandisha nguzo za Ghorofa ya kwanza hadi kupaua”. Alisema Askofu Mussa Mzumbi.