CCM: Shahada hii kwa Samia ni udhibitisho wa kazi anazofanya

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM)  kimesema kimeguswa na kufurahishwa na uamuzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kumtunuku shahada ya heshima ya udaktari wa falsafa Mwenyekiti wa  chama hicho, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan.

RAIS Samia, ametunukiwa shahada hiyo ya udaktari wa heshima leo Novemba 30, 2022 jijini Dar es Salaam katika  mahafali ya 52 duru ya 5 ya chou hicho.

Advertisement

Maazimio ya Seneti ya |Baraza la UDSM yalipitishwa katika kikao cha 876 ambapo yalimpendekeza Rais Samia kutunukiwa digrii hiyo ya juu ya heshima ya falsafa kwa kile walichoeleza kuwa uongozi wa Rais Samia pamoja na mambo mengine ameleta mageuzi ya kiuchumi pia umeleta tumaini jipya.

Rais Samia amesemwa kuboresha elimu ikiwemo kujenga vyuo 25, kusaini na benki ya dunia mradi wenye thamani ya bililioni zaidi ya 900 wenye lengo la kuboresha elimu ya juu.

Akizungumza saa chache baada ya Rais Samia kutunukiwa shahada hiyo, Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM  Taifa, Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka amesema uamuzi wa Chuo Kikuu cha UDSM kumtunuku Rais Samia shahada ya heshima ni uthibitisho wa dhahiri wa kazi kubwa na nzuri zinazofanywa na serikali ya CCM, awamu ya sita chini ya uongozi wa Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuleta ustawi wa maisha na maendeleo endelevu kwa nchi.

“Kati ya kazi kubwa zlizofanyika na kutumika kumtunuku shahada hiyo ya heshima ni pamoja na mageuzi ya kiuchumi, uimarishaji wa misingi ya demokrasia, utawala bora, maendeleo ya jamii, ameleta furaha na tumaini jipya miongoni mwa wananchi.” Amesema Shak ana kuongeza

“Mambo yote haya  ni utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM 2020-2025 uliochagizwa na utashi wake wa kisiasa, ukomavu na umahiri alionao katika uongozi wake.”Amesema

Amesema shahada hiyo ya heshima ni fahari kwa  Chama Cha Mapinduzi  na watanzania wote kuwa tunaye Rais anayewajibika kwa maslahi ya wote na tunaimani ya kwamba itampa moyo kuwa watanzania wanaona kazi nzuri anazozifanya kwa Taifa hivyo kumpa ari na nguvu ya kuendelea kutekeleza wajibu wake.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *