Shangwe zatawala Naibu Waziri Mkuu bungeni

SHANGWE zimetawala bungeni, wakati Naibu Waziri Mkuu, Dk Dotto Biteko alipokuwa akiingia bungeni leo mjini Dodoma baada ya kuapishwa Ijumaa iliyopita kushika wadhifa huo.

Wakati Dk Biteko akiingia saa 3;45 asubuhi, Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Ridhiwani Kikwete alikuwa akijibu swali la nyongeza katika wizara yake, lakini ghafla ukumbi ulianza kusikika shangwe za wabunge, hivyo kulazimika kutulia kidogo.

Spika wa Bunge Dk Tulia Ackson baada ya shangwe hizo kutulia, aliwashukuru wabunge kwa ukaribisho huo na kusema atatoa saamu za ukaribisho baadaye.

Habari Zifananazo

3 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button