Sheikh Jassim ajiondoa kuinunua Manchester United

#MICHEZO: ALIYEKUWA Waziri Mkuu wa Qatar tajiri, Hamad Jassim Jaber amejiondoa kwenye mchakato wa kuinunua klabu ya Manchester United kutoka kwa wamiliki familia ya Glazers.

Taarifa ya mwandishi wa habari za michezo kutoka Italia, Fabrizio Romano imeeleza baada ya majadiliano ya pande zote mbili, Glazers walikataa kuiuza klabu hiyo, na hivyo Sheikh Jassim kujiondoa.


Romano kwenye ukurasa wake wa mtandao wa X amesema kuwa zabuni ya mwisho ilikadiriwa kuwa mara mbili ya hesabu ya soko ya $3.5B.

Aidha katika taarifa hiyo, imeelezwa kuwa Sheikh Jassim alikuwa tayari kufanya uwekezaji wa ziada wa $1.5B.

Mara kadhaa familia ya Glazers imekuwa ikakataa kuiuza timu hiyo kwa tajiri huyo kutoka Qatar.

Habari Zifananazo

Back to top button