Shekhan Rashid kafiwa na baba yake
DAR=ES=SALAAM : Mchezaji wa zamani wa Klabu ya Simba Sports Club na Moro United Shekhan Rashid amefiwa na baba yake mzazi Rashid Abdallah aliyefariki leo jijini Dar-es-salaam katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Shughuli za maziko zitafanyika adhuhuri katika msikiti wa Al Maamur na baadaye Mzee Rashid Abdallah atazikwa katika makaburi ya Kisutu jijini Dar-es-salaam.
SOMA : Simba hawataki mchezo Misri
Shekhan Rashid ni miongoni mwa wachezaji waliopata nafasi ya kuchezea soka la kulipwa nchini Sweden.
SOMA: SHEKHAN RASHID: Tunawatengenezea mchongo wa Ulaya wachezaji wa Tanzania