Sherehe za Muungano zanoga Sumbawanga

RUKWA; WANAFUNZI wa shule mbalimbali za sekondari na msingi Manispaa ya Sumbawanga wamejitokeza kwa wingi katika kuadhimisha miaka 61 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Wanafunzi hao pia waliungana na watendaji mbalimbali serikalini kufanyw usafi kabla ya kuhudhuria mkutano wa hadhara uliofanyika ndani ya Kituo cha Mabasi cha Soko Matola kilichopo Kata ya Katandala.

Katika maadhimisho hayo Mkuu wa Mkoa Rukwa, Makongoro Nyerere amewataka wakazi wa mkoa huo na Watanzania kwa ujumla kuendelea kuuenzi na kudumisha Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ambao ni Tunu ya Taifa .

Anasema Muungano huo ambao umetimiza miaka 61 ni kielelezo tosha cha mshikamano, amani na umoja na usalama wa Watanzania bila kujali itikadi zao za kisiasa,imani zao za dini wala ukabila wao.

Katika hotuba iliyotolewa kwenye mkutano wa hadhara kwa niaba yake na Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga , Nyakia Chirukile, aliwataka wakazi wa mkoa huo kuhakikisha wanaendelea kuilinda amani wakati wakisheherekea miaka 61 ya Muungano huo.

Awali kabla ya hotuba hiyo, wanafunzi na baadhi ya watendaji serikalini walifanya shughuli ya usafi kwenye Barabara ya Two Way, huku kivutio kikubwa kikiwa wanafunzi kutokana na sare zao tofauti za shule zenye rangi tofauti.

 

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button