INEC yataja utaratibu wa kugombea urais

DODOMA: SHERIA ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani Namba 1 ya mwaka 2024 inataka mgombea wa urais kuwasilisha fomu za uteuzi si zaidi ya saa 10 alasiri siku ya uteuzi. Sheria hiyo inaeleza fomu ya uteuzi lazima iwe na jina la mgombea, jinsi, hali ya ulemavu (ikiwa ipo), anuani na taarifa za mgombea mwenza. Pia, fomu hiyo inapaswa kuwa na tamko la mgombea kuthibitisha yupo tayari na ana sifa za kugombea.

Sheria inataka kiapo cha mgombea wa urais na makamu wake kijazwe na kusainiwa mbele ya jaji. Aidha, lazima iambatane na majina ya wadhamini, namba za kadi za kura na uthibitisho wa msimamizi wa uchaguzi. Kanuni za uchaguzi zinabainisha kuwa endapo Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) itaridhika mgombea amekidhi vigezo, itathibitisha uteuzi wake kupitia Fomu Na. 8A.

Pingamizi
Kanuni hizo pia zinaeleza kuwa pingamizi linaweza kuwasilishwa na mgombea mwingine, Msajili wa Vyama vya Siasa au Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Pingamizi la Msajili litahusu Sheria ya Gharama za Uchaguzi pekee, huku pingamizi la mgombea au Mwanasheria Mkuu likitakiwa kuwasilishwa si zaidi ya saa 10 alasiri siku inayofuata ya uteuzi.

Kanuni zimeeleza kuwa endapo Tume itakubali pingamizi, jina la mgombea husika litaondolewa kwenye orodha ya wagombea walioteuliwa. SOMA: CCM yafunika Dar, Samia aahidi makubwa siku 100 ofisini

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button