Shigongo ahoji utaratibu kurejeshwa RPL

DODOMA; MBUNGE wa Buchosa, Eric Shigongo amehoji bungeni ni lini serikali itarejesha utaratibu wa kutambua Maarifa Nje ya Mfumo Rasmi (RPL).

Akijibu swali hilo. Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Omari Kipanga amesema: “Kwa sasa Serikali imeandaa Mwongozo wa Kutathmini na kutambua Maarifa yaliyopatikana nje ya Mfumo Rasmi (Recognition of Prior Learning).

“Mwongozo unaweka utaratibu wa utambuzi na urasimishaji wa maarifa yaliyopatikana nje ya mfumo wa shule katika fani mbalimbali za amali kwa lengo la kuwawezesha walengwa kushiriki kikamilifu katika ulimwengu wa kazi.

“Kwa kuzingatia maelekezo ya Sera ya Elimu na Mafunzo 2014, toleo 2023, ambapo mfumo wa kutambua na kurasimisha ujuzi na stadi zinazopatikana nje ya mfumo rasmi wa elimu na mafunzo umepewa kipaumbele.

“Serikali itatekeleza afua za kuimarisha utaratibu wa utambuzi na urasimishaji wa maarifa, ujuzi na stadi zinazopatikana nje ya mfumo rasmi wa elimu na mafunzo.

“Aidha, elimu nje ya mfumo rasmi itatambuliwa, na watakaopitia mfumo huo watakuwa na fursa ya kujiunga na mfumo rasmi wa elimu kulingana na vigezo vitakavyowekwa,” amesema.

Habari Zifananazo

Back to top button