Shirika lawakumbuka vijana ujenzi wa taifa
DAR ES SALAAM: SHIRIKA la Vijana Tai Tanzania kwa kushirikiana na ubalozi wa Marekani nchini Tanzania wataendelea kuwezesha vijana wengi kupata taarifa muhimu kupitia njia mbalimbali ikiwa ni pamoja na hadithi, filamu na simulizi hali itakayotoa fursa kwa vijana hao kupata maarifa sahihi katika kuchagiza maendeleo ya taifa
Ofisa Mawasiliano na Mahusiano Kutoka Tai Tanzania, Emmyrose Rugumamu amesema hayo alipozungumza na wanahabari mara baada ya zoezi la uoneshaji wa filamu ya Kimarekani inayohamasisha matumizi ya teknolojia katika kuleta maendeleo ambapo mpaka sasa mradi huo umefikia vijana zaidi ya 500 na kuwapa elimu ya masuala.
Ofisa utamaduni kutoka ubalozi wa Marekani nchini Tanzania, Chad Morris amebainisha kuwa vijana wana nafasi kubwa katika kuchochea maendeleo ya taifa hivyo ni vyema kwa wadau kutumia njia mbalimbali za kuwaelimisha.
SOMA: Mabadiliko ya mfumo yarahisishwa kwa vijana
Josephine Lawi ambaye ni Mkurugenzi wa Shirika la Step Step foundation ameiomba Tai Tanzania kuongeza juhudi katika utoaji wa elimu kama hiyo hususa ni kwa vijana waliopo gerezani huku mmoja wa wanafunzi walioshiriki zoezi hilo akiiomba serikali kushirikiana na wadau mbalimbali katika kuhakikisha elimu hiyo inafika kwa wanafunzi wengi zaidi na hivyo kuwaongezea uelewa.