Mabadiliko ya mfumo yarahisishwa kwa vijana

DAR-ES-SALAAM: Mashirika ya vijana, wadau wa maendeleo na serikali walikutana jijini Dar es Salaam kujadili jinsi vijana wanavyoweza kukabiliana na mabadiliko ya kiuchumi na changamoto za sheria na sera zinazohusu mashirika ya vijana.

“Tumejadili mabadiliko ya sheria na miongozo iliyotolewa na serikali kuimarisha mazingira ya uendeshaji wa mashirika ya vijana,” alisema Charles Komba,

SOMA:Tanzania kidedea Mashindano ya TEHAMA China

Advertisement

Afisa Ufuatiliaji na thamani  na  Mwandamizi kutoka Ofisi ya Msajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali. Ameelezea pia changamoto kama vile uanzishwaji wa Baraza la Taifa la Vijana na upatikanaji wa misamaha ya kodi.

Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Tanzania Bora Initiative, aliongezea kuwa “Tunazingatia jinsi ya kuleta mabadiliko ya sheria na sera zitakazoboresha uwezo wa mashirika ya vijana kutoa mchango chanya katika maendeleo ya taifa.”alisema.

SOMA: https://news.un.org/sw/story/2024/07/1177466

Nasibu Richard, Ofisa Mwandamizi kutoka Idara ya Maendeleo ya Vijana – Ofisi ya Waziri Mkuu, alihitimisha kwa kusema: “Mwitikio wa vijana katika fursa za kitaifa na kimataifa umekuwa mkubwa, na ushiriki wao unaendelea kuimarika kufuatia sera za Rais Samia za kuwapa nafasi vijana kushiriki katika maendeleo ya nchi.”