Shughuli za kiuchumi zisiathiri malezi – RAS Songwe

KATIBU Tawala Mkoa wa Songwe, Happness Seneda amewataka wazazi, walezi na jamii kwa ujumla kujikita katika malezi bora ya watoto badala ya kusingizia ubize wa shughuli za kiuchumi.

Amezungumza hayo katika kikao cha mapitio ya utekelezaji wa Program Jumuishi ya Malezi Makuzi na Maendeleo ya awali ya Mtoto PJMT MMMAM robo ya kwanza ngazi ya mkoa kilichofanyika Aprili 29,2025 Songwe.

Amesema wazazi na walezi wengi mkoani Songwe wamejikita zaidi katika shughuli za kiuchumi hasa biashara, kilimo uchimbaji na ufugaji , huku wakisahau suala la malezi ya watoto, jambo ambalo limekuwa na madhara mengi ya matukio mengi ya ukatili kwa watoto wadogo kuanzia miaka mitano kutokana na kutokuwa karibu nao.

“Shughuli za kiuchumi zimekuwa zikuchua nafasi kubwa sana kuliko kuangalia malezi ya watoto, madhara yake vitendo vingi vya unyanyasaji vimekuwa vingi zikiwemo mimba za utotoni ambapo mkoa wetu unaongoza kwa mujibu wa utafiti wa afya ya uzazi na mtoto (TDHS), zaidi ya 45% ya wasichana chini ya miaka 18 wanapata mimba katika mkoa wetu,” amesema Seneda.

Amesema malezi ya watoto yanahitaji ukaribu wa wazazi walezi kuwa karibu na watoto hasa wenye umri chini ya miaka nane ili kuweza kujua mahitaji yao na kutambua baadhi ya changamoto wanazo kutana nazo wakiwa shuleni au katika mazingira yanayowazunguka.

Seneda pia amewaagiza maafisa ustawi kuhakikisha wanahakiki vituo vya kulelea watoto mchana katika halmashauri zote kuhakikisha vinakizi vigezo kwa kuwa na miundo mbinu rafiki kwa watoto ambayo imepitishws na kupendezwa na serikali

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button