Shule 19 zapatiwa vifaa vya Tehama

SHULE 19 za msingi na sekondari katika mikoa tisa nchini zimepokea vifaa vya TEHAMA vyenye thamani ya Shilingi milioni 769, hatua inayotarajiwa kuboresha ufundishaji wa masomo ya sayansi na teknolojia pamoja na kuongeza uelewa wa wanafunzi kupitia ujifunzaji wa vitendo.
Akizungumza katika hafla ya ugawaji wa vifaa hivyo leo, Machi 30, 2026, Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Wanu Hafidh Ameir, alisema vifaa hivyo ni sehemu ya utekelezaji wa mkakati wa Serikali wa kuimarisha matumizi ya teknolojia za kidijitali katika elimu, kwa lengo la kuongeza ubora na ufanisi wa ujifunzaji. SOMA: IAA yawekeza bilioni mbili kwenye teknolojia

Amebainisha kuwa kupitia uwekezaji huo, walimu watanufaika kwa kutumia mbinu bunifu za kufundishia, huku wanafunzi wakipata fursa ya kujifunza kwa kuona na kufanya, jambo litakalosaidia kukuza ubunifu, ujuzi wa TEHAMA na kuendana na mahitaji ya soko la ajira la sasa. “Leo tumegawa vifaa hivi; niombe visifungiwe kabatini. Vitunzeni na vitumike kwa muda mrefu ili viwanufaishe wanafunzi wengi,” alisisitiza Ameir.
Mbali na ugawaji huo, Serikali imeendelea kuwekeza katika miundombinu ya elimu ya kidijitali kwa kuanzisha madarasa janja matano na kufunga mbao janja 422 katika shule za sekondari, sambamba na utekelezaji wa mkakati wa kitaifa wa matumizi ya TEHAMA na Akili Unde (AI) katika elimu.




JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 12000-16700 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..
.
This is my main concern…………………… http://Www.Cash54.Com
I just came across this amazing way to earn $11,000-$15,000 a month online! No selling, no struggle—just a simple system that anyone can follow. Mia Westbrook did it, and so can you! Don’t miss out on this life-changing opportunity.
.
This is what I do…………………… http://Www.Payathome9.Com