Tanzania, A. Kusini zaweka mkazo ufundishaji Kiswahili

CAPE TOWN, AFRIKA KUSINI: Tanzania na Afrika Kusini zimeongeza juhudi za kutekeleza Hati ya Makubaliano (MoU) ya mwaka 2022 kuhusu ushirikiano katika elimu ya msingi, kwa lengo la kukuza ufundishwaji wa lugha ya Kiswahili katika shule za Afrika Kusini.

Mnamo Agosti 2022, nchi hizo mbili wanachama wa SADC zilitia saini makubaliano hayo kama sehemu ya juhudi za kukuza lugha hiyo na ushirikiano wa kikanda.

Suala hilo limeibuka leo, Machi 24, 2026, jijini Cape Town, Afrika Kusini, wakati Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia wa Tanzania, Wanu Hafidh Ameir, alipokutana na Naibu Waziri wa Sayansi, Teknolojia na Ubunifu wa Afrika Kusini, Dk Nomalungelo Gina, kujadili masuala mbalimbali yenye lengo la kuimarisha sekta ya elimu katika nchi hizo mbili.

Katika mkutano huo, Wanu alieleza hatua mbalimbali zinazochukuliwa na Serikali ya Tanzania katika kuboresha elimu, sayansi na teknolojia.

Kuhusu Kifungu cha 9 cha MoU, viongozi hao wawili walisisitiza umuhimu wa utekelezaji madhubuti wa kifungu hicho ili kukuza Kiswahili kimataifa na kuimarisha mshikamano wa kikanda kupitia elimu.

Kupitia mazungumzo hayo, Tanzania na Afrika Kusini zimekubaliana kuimarisha ushirikiano katika sekta ya elimu, ikiwemo kupanua programu za ubadilishanaji wa walimu na wataalamu katika elimu, sayansi, teknolojia na ubunifu, pamoja na kuendeleza mafunzo ya ufundi stadi.

Maeneo mengine ni pamoja na kuimarisha programu za tafiti, kuendeleza ushirikiano kati ya taasisi na vyuo vya elimu ya juu, pamoja na kuongeza fursa za ufadhili wa masomo.

SOMA: Watengeneza maudhui ya Kiswahili kulipwa

Serikali ya Tanzania pia imeeleza dhamira yake ya kupanua fursa kwa vijana wa Kitanzania wanaonufaika na programu mbalimbali za ufadhili wa masomo, ikiwemo Samia Scholarship.

Pande zote mbili pia zimesisitiza umuhimu wa kuendeleza programu za pamoja zitakazochochea ubunifu, uhamishaji wa teknolojia na kuboresha ubora wa elimu katika nchi zote mbili.

Naibu Waziri wa Tanzania pia alithibitisha dhamira ya Serikali ya Tanzania ya kuendelea kuboresha mifumo ya elimu ili kukidhi mahitaji ya uchumi wa kisasa, huku akitambua mchango wa ushirikiano wa kimataifa katika kufanikisha azma hiyo.

Kwa upande wake, Dk Gina alieleza utayari wa Afrika Kusini kuendelea kushirikiana na Tanzania katika maeneo ya kipaumbele, ikiwemo tafiti za kisayansi, maendeleo ya ujuzi kwa vijana na matumizi ya teknolojia katika ufundishaji na ujifunzaji.

Viongozi hao pia walibadilishana uzoefu kuhusu sera, mikakati na mifumo ya usimamizi wa elimu, sayansi na teknolojia, pamoja na kujadili njia bora za kukabiliana na changamoto zinazoikabili sekta hiyo katika mazingira ya dunia yanayobadilika kwa kasi.

Habari Zifananazo

3 Comments

  1. I get paid more than $120 to $130 per hour for working online. I heard about this job 3 months ago and after joining this i have earned easily $15k from this without having online working skills.
    Here is I begun— http://www.giftpay7.vip

  2. JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 12000-16700 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..
    .
    This is my main concern…………………… http://Www.Cash54.Com

  3. I just came across this amazing way to earn $11,000-$15,000 a month online! No selling, no struggle—just a simple system that anyone can follow. Mia Westbrook did it, and so can you! Don’t miss out on this life-changing opportunity.
    .
    This is what I do…………………… http://Www.Payathome9.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button