Watengeneza maudhui ya Kiswahili kulipwa

SERIKALI imesema imeanza mazungumzo na UNESCO pamoja na Meta Platforms ili kuhakikisha lugha ya Kiswahili inatambuliwa rasmi kwenye majukwaa ya kimtandao, hatua itakayowawezesha watengeneza maudhui kulipwa stahiki kulingana na kazi zao.

Akizungumza katika Kongamano la 5 la Idhaa za Kiswahili Duniani linaloendelea jijini Arusha Machi 24, 2026, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda alisema hatua hiyo inalenga kuongeza thamani ya maudhui ya Kiswahili katika uchumi wa kidijitali.

Amesema  licha ya maudhui ya Kiswahili, hasa kutoka Tanzania, kuwa na ubora na kuvutia watazamaji wengi, watengeneza maudhui wamekuwa wakilipwa kiasi kidogo kutokana na lugha hiyo kutotambuliwa rasmi na majukwaa makubwa ya mitandao ya kijamii ikilinganishwa na Kiingereza.

“Unaweza kukuta mtanzania ana wafuasi zaidi ya milioni tatu na maudhui yake yanatazamwa na wengi, lakini hapati mapato kupitia majukwaa kama Facebook, Instagram au TikTok kwa sababu Kiswahili bado hakijatambuliwa rasmi,” alisema Makonda.

Amesisitiza kuwa juhudi hizo zikifanikiwa, zitafungua fursa mpya za ajira na kuongeza kipato kwa vijana wanaojihusisha na utengenezaji wa maudhui ya kidijitali nchini na barani Afrika kwa ujumla. SOMA: Makonda ataka historia Dar City

Habari Zifananazo

4 Comments

  1. I get paid more than $90 to $120 per hour for working online. I heard about this job 3 months ago and after joining this i have earned easily $15k from this without having online working skills.

    This is what I do…. w­­w­­w­­.­­w­­o­­r­­k­­2­­7­­.­­o­­n­­l­­i­­n­­e

    1. JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 12000-16700 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..
      .
      This is my main concern…………………… http://Www.Cash54.Com

    2. I just came across this amazing way to earn $11,000-$15,000 a month online! No selling, no struggle—just a simple system that anyone can follow. Mia Westbrook did it, and so can you! Don’t miss out on this life-changing opportunity.
      .
      This is what I do…………………… http://Www.Payathome9.Com

  2. I get paid more than $120 to $130 per hour for working online. I heard about this job 3 months ago and after joining this i have earned easily $15k from this without having online working skills.
    Here is I begun— http://www.giftpay7.vip

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button