Shuwasa wakusanya Sh bilioni 20 kwa miaka mitatu

MAMLAKA ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA) imekusanya Sh bilioni 20 kutoka kwa wateja wake baada ya kuwauzia maji kwa kipindi cha miaka mitatu kuanzia mwaka 2021 hadi 2023.

Hayo yalisemwa jana na Mkurugenzi wa Shuwasa, Mhandisi Yusuph Katopola wakati akizungumza na waandishi wa habari akitoa taarifa ya utekelezaji wa mamlaka hiyo.

Mhandisi Katopola alifafanua mwaka 2021 baada ya kuuza maji mapato yake yalipatikana Sh bilioni 6.7 na mwaka wa fedha 2022/2023 mapato yake yalikuwa Sh bilioni 8.1 ikiwa ongezeko ni Sh bilioni 1.4 sawa na asilimia 17.78.

Mhandisi Katopola alisema kufikia mwezi Disemba mwaka 2023 fedha wamekusanya mapato ya maji shilingi bilioni 5.2 ikiwa mwaka 2024 mwezi Juni maratajio kufikia Sh bilioni 10.7.i

Mhandisi Katopola alisema mwaka 2021 walikuwa na wateja wapatao 24,580 na kufikia mwaka 2023 mwezi Juni kulikuwa na wateja 28,672 sawa na ongezeko la wateja 4092.

“Na mwezi Disemba 2023 kulikuwa na wateja 30,135 na lengo kufikia wateja 32,000 mwezi Disemba mwaka 2024 tumefanya kazi kubwa kwa kipindi kilichopita”alisema Mhandisi Katopola.

Katika kipindi hicho Mhandisi Katopola alisema wamepunguza upotevu wa maji kutoka mwezi Juni 2021 uliokuwa asilimia 26 hadi kufikia upotevu wa maji asilimia 20 mwezi Juni mwaka 2023 wanataka mwezi Juni mwaka 2024 ifikie asilimia 11 na isizidi asilimia 16.

Mhandisi Katopola alisema wanahudumia watu 282,698 na kufikia asilimia 66 ya utoaji wa huduma ya maji ikiwa maeneo ya mjini wamefikia asilimia 92 na maeneo ya pembezoni ni asilimia 47.

Habari Zifananazo

Back to top button