- USHINDI au sare ya bila kufungana, itawapeleka Simba SC katika hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika, baada ya mchezo wa leo kuisha sare ya mabao 2-2 dhidi ya Power Dynamos nchini Zambia.
–
Simba itarudiana na timu hiyo Septemba 30, Dar es Salaam.
–
Katika mchezo huo, wenyeji Dynamos walianza kutangulia kwa bao lililofungwa na Joshua Mutale dakika ya 29, bao hilo lilidumu hadi mapumziko.
–
Dakika ya 60 Clatous Chama alisawazisha bao hilo na kuwa 1-1, kabla ya dakika ya 75 Cephas Mulombwa kuifungia Dynamos bao la pili.
–
Dakika za mwisho Chama alifunga tena na ubao kusomeka 2-2.
–
Wakati huohuo Yanga imepata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya El-Merreikh ikiwa ugenini.
–
Mabao ya Yanga yalifungwa na Kenneth Musonda dakika ya 63 na Clement Mzize dakika ya 80.
–
Sare yoyote itawavusha Yanga kwenda hatua ya makundi.
Back to top button