Simba mguu moja makundi shirikisho

DAR ES SALAAM: Leonel Ateba ndiye aliyefufua matumaini ya Simba SC kwenda makundi ya Kombe la Shirikisho baada ya kuweka msumari wa pili, dakika chache baada ya Kibu Denis kusawazisha bao la uongozi wa Al-Ahli Tripol, na sasa ni mapumziko.

Mchezo huo ni raundi ya pili unaopigwa uwanja wa Mkapa, Simba imeenda mapumziko ikiwa mbele mabao 2-1.

Uongozi huo ni ishara njema kwa Simba kwani tayari mguu mmoja umetangulia hatua ya makundi Kombe la Shirikisho, endapo mchezo ukiisha hivyo, Simba watakuwa wamefunzu makundi.

Advertisement

Al Ahli walikuwa wa kwanza kupata bao lililofungwa na Agostinho Mabululu, kabla ya Kibu Denis kusawazisha na Leonel Ateba kuweka msumari wa pili.