Simba: Tulipambana bahati haikuwa kwetu

MISRI: KLABU ya Simba imeeleza kuwa haikuwa bahati kwao kufuzu nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika licha ya wachezaji wa timu hiyo kumwaga jasho jingi kwa ajili ya nembo ya timu yao .
Simba imeondoshwa na Al Ahly kwa jumla ya mabao 3-0 baada ya jana usiku kukubali kichapo cha mbao 2-0 huko nchini Misri katika mchezo wa robo fainali mkondo wa pili.
Kupitia ukurasa wa Instagram wa timu hiyo wamechapisha ujumbe wenye kutia moyo wachezaji pamoja na mashabiki wa Simba huku wakipania michuano mingine iliyosalia.
 
“Mashujaa wetu walipambania nembo ya Simba na Tanzania lakini bahati haikuwa kwetu. Kimataifa tumemaliza lakini mashindano ya ndani yanaendelea, nguvu zetu tunahamishia huko ili kufanya vizuri.”
Kuondoshwa kwa Simba kwenye michuano hiyo kunaacha pigo kwenye soka la Tanzania baada ya siku hiyohiyo Yanga kutupwa pia nje ya michuano hiyo na Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini, hivyo kulifanya taifa kukosa uwakilishi kwenye hatua ya nusu fainali.

Habari Zifananazo

Back to top button