Simba wapewa chao ahadi ya Samia

SIMBA SC wamekabidhiwa Sh milioni 5 baada ya kupata bao moja katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika waliopoteza mabao 3-1 dhidi ya Raja Casablanca usiku wa kuamkia jana, ikiwa ni mwendelezo wa ahadi ya Rais Samia Suluhu Hassan ya kununua kila bao.

Bao la Simba lilifungwa na Jean Baleke likihakikishia timu hiyo kupata Sh 5 milioni ambayo imekabidhiwa leo Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa.

Kwa ujumla Simba katika hatua ya makundi imebeba Sh 50 milioni za Rais Samia imefunga mabao 10, saba ikimfunga Horoya, mawili Vipers na moja Raja.

Kikosi hicho kimetua jijini Dar es Salaam leo kutoka Morocco na sasa kinasubiri ratiba ya robo fainali itakayotolewa Jumatano hii.

Habari Zifananazo

Back to top button