Simba watangulia robo fainali

SIMBA SC imetangulia robo fainali ya Kombe la Azam, baada ya ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya African Sports ya Tanga mchezo uliopigwa Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam.

Mabao ya Simba yamefungwa na Jean Baleke dakika ya 36, Kennedy Juma dakika ya 47, Mohammed Mussa dakika ya 69 na Jimmyson Mwanuke dakika ya 90.

Baada ya kutangulia hatua hiyo, Simba itasubiri droo ya mchezo wa robo fainali.

Watani wao Yanga wanakipiga kesho dhidi ya Tanzania Prison katika Uwanja wa Azam uliopo Chamazi Dar es Salaam.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button