Simba yanasa kipa mpya kutoka Morocco
KLABU ya Simba imethibitisha kukamilisha usajili wa kipa, Ayoub Lakred kutoka FAR Rabat ya Morocco.
Lakred (28) amesaini mkataba wa miaka miwili.
Kipa huyo ameiongoza FAR Rabat kushinda ubingwa wa Ligi Kuu ya Morocco na kuifikisha Nusu fainali ya CAFCC.