Simba yapoteza Misri

MISRI; SIMBA imekubali kipigo cha mabao 2-0 kutoka kwa Al Masry ya nchini Misri katika mchezo wa robo fainali ya kwanza Kombe la Shirikisho Afrika mchezo uliofanyika leo Aprili 2, 2025 Uwanja wa Uwanja wa Suez Canal nchini humo.

Timu hizo zitarudiana wiki ijayo Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam, ambapo ili isonge mbele Simba itatakiwa ishinde mabao 3-0.

Hii ni robo fainali ya sita kwa Simba katika michuano ya CAF katika misimu saba kuanzia 2018/2019 na hakuna hata moja aliyovuka baada ya kushindwa kupata ushindi ugenini, lakini wiki iliyopita walizindua kauli mbiu yao isemayo: ‘Hii Tunavuka’.
–



