Simba yasaini mkataba udhamini timu ya vijana

SIMBA SC imesaini mkataba wa udhamini wa miaka miwili kwa ajili ya kuendeleza soka la vijana wenye thamani ya Sh milioni 500 na kampuni ya MobiAd leo.

Akizungumza kuhusu udhamini huo, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, Salim Abdallah ‘Try Again’ amesema timu hiyo inalenga kuboresha soka la vijana, wakati huohuo, rais wa heshima wa timu hiyo, Mo Dewji amekubali kuendeleza soka la vijana.

“Tuna malengo ya kuboresha soka la vijana, shamba ambalo tunajua litatusaidia kuvuna vipaji kwa ajili ya timu ya wakubwa. Hivi karibuni tutaanza ujenzi wa kituo chetu.” ‘Try Again’.

‘Try Again’ amewashukuru MobiAd kwa kukubali kudhamini timu ya vijana, ambapo ameongeza kuwa “kama Simba SC tunawaahidi kwamba fedha hizi zitatumika vizuri kwani vijana ndio msingi wa timu yetu”.

Habari Zifananazo

Back to top button