Simba yatangaza vita ya ubingwa

TIMU ya Simba imekuja na kampeni ya kutafuta pointi 30 katika michezo 10 iliyobaki kushinda ubingwa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Simba inashika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi hiyo ikiwa imecheza mechi 20 na kujikusanyia pointi 51 ikiwa na mchezo mmoja mkononi.

Akizungumza Dar es Salaam hivi karibuni, Meneja wa Habari na Mawasiliano wa timu hiyo, Ahmed Ally alisema timu hiyo inatafuta pointi 30 katika michezo 10 iliiyosalia kushinda ubingwa.

“Sisi tunatambulisha kampeni yetu rasmi katika mechi yetu dhidi ya Coastal, tunaanza kampeni ya kutafuta alama 30 katika mechi 10 iliyosalia. Raundi ya pili kila mtu anacheza kwa malengo hakuna timu inayocheza kukamilisha ratiba na hiyo inafanya ligi kuwa ngumu,” alisema Ahmed.

Sambamba na hilo alisema kwa sasa hawana shinikizo lolote kwa pointi walizopitwa na Yanga, bali hesabu zao zipo katika michezo 10 iliyosalia.

“Kupitwa na anayeongoza ligi haitupi shinikizo bali inatupa umakini wa kuendelea kupambana zaidi, zimebaki mechi 10 ndiyo zenye thamani kubwa,” aliongezea Ahmed.

Timu hiyo itakuwa mgeni wa Coastal Union, Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha majira ya saa 10:00 jioni.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button