Simbachawene aonya maadili yasiyofaa kwa Watumishi

ARUSHA: WAZIRI wa nchi, Ofisi ya rais, menejimenti ya utumishi wa umma na utawala bora, George Simbachawene amewaonya Watumishi wanaokosa maadili katika utumishi wa umma kwenye maeneo mbalimbali.

Ameyasema hayo katika ufunguzi wa kikao kazi cha Wakuu wa idara za utawala na rasilimaliwatu katika Wizara,idara zinazojitegemea, Wakala, Taasisi za umma,sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za serikali za mitaa kinachofanyika katika kituo cha Mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC) ambapo amesisitiza Watumishi kusimama katika misingi ya maadili ya kazi.

Amewataka Watumishi kuwa na Utumishi wenye tija pamoja na utekelezaji wa miundo na mifumo ya uendeshaji na utoaji huduma kwani majukumu hayo ni makubwa na muhimu katika kuhakikisha taasisi yoyote ya Umma inakuwa na tija kwa Taifa.

Simbachawene amesema Watumishi wanapaswa kuzingatia umuhimu wa maadili kwani ofisi yake imeendeleea kupokea malalamiko kuhusu vitendo vya uvunjifu wa maadili ikiwemo Rushwa.

Amesema pia ukosefu wa maadili umepelekea watumishi kuwa na lugha zisizofaa, kufanya udanganyifu wa nyaraka ikiwemo kughushi barua za masuala mbalimbali ya kiutumishi kama uhamisho wa kwenda sehemu zenye maslahi mazuri.

“Wote wanao jihusisha na tabia hii kuacha mara moja na hatua kali zitaendelea kuchukuliwa kwa wahusika”amesisitiza.

Akizungumzia suala la uhamisho kwa Watumishi amesema kumekuwepo tabia ya baadhi ya waajiri kukataa kuwapokea watumishi wanaohamishiwa kwenye taasisi hizo na kutoruhusu watumishi kuhama hata pale inapoelekezwa na mamlaka.

Ameesema vitendo hivyo ni kinyume na Sheria, Kanuni na taratibu kwa kuwa kitendo hicho ni kukosa utii na amewaelekeza waajiri wa aina hii waache tabia hizo.

“Maadili ni msingi wa utendaji kazi katika Utumishi wa Umma, Utafiti wa hali ya uzingatiaji wa maadili katika ofisi ya wa Umma uliofanywa mwaka 2022 ulibaini uwepo wa vitendo visivyo vya kiuadilifu katika Utumishi wa Umma ikiwemo matumizi mabaya ya madaraka kwa manufaa binafsi, mgongano wa kimaslahi na matumizi mabaya ya mamlaka,”amesema Simbachawene

“Mtumishi anayeharibu achukuliwe hatua za kinidhamu mahali alipo na siyo kukimbilia kumhamisha na nasisitiza kuendelea kusimamia, kuboresha utendaji na pale ambapo tutabaini mapungufu kuanzia sasa tutachukua hatua stahiki”ameongeza Simbachawene.

Aidha katika hatua nyingine ameeleza kuwa hivi karibuni Serikali kupitia Ofisi yake ilitoa vibali vya kuwapandisha madaraja watumishi wa Umma 120,210 na kuwabadilisha Kada Watumishi 8,080 na kusema pia Serikali imetoa nyongeza ya mwaka ya mshahara kwa watumishi wake na itaendelea kuboresha maslahi ya watumishi kulingana na uwezo wa uchumi.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
2 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
angliacoolidge
angliacoolidge
1 month ago

While studying full-time, I’ve earned $64,000 USD so far this year. I’m making a lot of money using an online business idea I found. It’s quite user-friendly, and I’m delighted I found it.
.
.
Detail Here——————————————————–>>>  http://Www.BizWork1.Com

Patrick
Patrick
1 month ago

Google pay 390$ reliably my last paycheck was $55000 working 10 hours out of consistently on the web. My increasingly youthful kinfolk mate has been averaging 20k all through continuous months and he works around 24 hours reliably. I can’t trust how direct it was once I attempted it out.(00q) This is my essential concern…:) GOOD LUCK
For more info visit………….. http://www.Smartcash1.com

Back to top button
2
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x