Simbachawene ashauri uwekezaji vituo vya mafuta vijijini

DODOMA: Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Simbachawene ameishauri Wizara ya Nishati kuendelea kuweka mazingira wezeshi yatakayowezesha uwekezaji zaidi wa vituo vya mafuta vijijini.
Simbachaene emetoa rai hiyo leo, 17 Juni, 2025, jijini Dodoma wakati alipotembelea banda la Wizara ya Nishati katika Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea katika viwanja vya Chinangali.
Maonesho hayo yamezinduliwa leo.
SOMA: Serikali: Jukumu la kupandisha vyeo watumishi ni la mwajiri
“Wafanyabiashara wengi wanataka kuwekeza kwenye vituo vya Mafuta vijijini kwakuwa bado kuna uhaba wa vituo, hivyo angalieni masharti yanayowekwa kwenye uwekezaji yasiwe kikwazo kwenye huduma hii muhimu,” Waziri amesema.
Aidha, Simbachawene ameishauri Wizara kuongeza kasi ya upatikanaji wa nishati safi ya kupikia hususani maeneo ya vjijini pamoja na kuhamasisha uwekezaji kwenye nishati safi ya kupikia.
Vilevile, ameipongeza Wizara ya Nishati na Taasisi zake kwa kazi kubwa wanayoifanya ya kuendelea kutoa huduma za Nishati kwa wananchi.