Singida Fountain Gate sasa kambi Arusha

TIMU ya Singida Fountan Gate imeamua kubadili uamuzi wa kambi ya maandalizi ya msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Awali timu hiyo ilipanga kuweka kambi nchini Tunisia lakini taarifa iliyotolewa leo Julai 7, 2023 imesema timu hiyo sasa itaweka kambi jijini Arusha.

Taarifa ya Singida iliyochapishwa kwenye kurasa zao za mitandao ya kijamii imetaja sababu ya kubadili uamuzi.

” Tunapenda kuwataarifu wadau na mashabiki wa klabu yetu ya Singida Fountain Gate kwamba maandalizi ya msimu ujao yatafanyika jijini Arusha kuanzia Julai 10, 2023.

Awali maandalizi yalikuwa yafanyike Tunisia lakini kutokana na ufinyu wa muda na kuchelewa kwa zoezi la usajili tumelazimika kubaki nchini”.

Singida Fountain Gate watashiriki michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika kwa mara ya kwanza.

Habari Zifananazo

Back to top button