SMZ kuimarisha mfumo kidigitali kudhibiti ajali

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Hussein Ali Mwinyi, amesema Serikali inaendelea kujipanga kuimarisha matumizi ya mifumo ya kidigitali ili kudhibiti vifo vinavyotokana na ajali pamoja na makosa ya barabarani.

Dk Mwinyi ametoa kauli hiyo leo Januari 06, 2026 alipokutana na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene, aliyefika Ikulu Zanzibar kwa mazungumzo ya kikazi.

Amesema kukamilika kwa mfumo huo wa kidigitali pamoja na matumizi ya taa za usalama barabarani (Traffic Lights) na uwekaji wa rada za kudhibiti kasi, kutasaidia kwa kiasi kikubwa kudhibiti makosa yanayofanyika barabarani, kupunguza vifo vinavyotokana na ajali pamoja na kupunguza gharama za huduma za afya zinazobebwa na Serikali baada ya ajali kutokea.

SOMA: Barabara kilomita 24.5 zafunguliwa Zanzibar

Akizungumzia suala la unyanyasaji na ukatili wa kijinsia, ikiwemo vitendo vya ubakaji, Dk Mwinyi amesema Serikali imechukua hatua madhubuti kudhibiti vitendo hivyo, ikiwemo kuondoa dhamana kwa watuhumiwa wa makosa hayo, pamoja na kuendelea kutoa elimu kwa umma dhidi ya udhalilishaji.

Akizungumzia matukio ya uhalifu na makosa katika maeneo ya utalii, amesema Serikali inaendelea kuchukua juhudi kubwa za kuimarisha usalama katika maeneo hayo, ikiwemo kuwataka wamiliki wa hoteli kuweka kamera za CCTV ili kusaidia kukabiliana na vitendo vya uhalifu.

Rais Mwinyi amepongeza ushirikiano uliopo kati ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, hususan katika kuimarisha utendaji wa pamoja wa sekta za Uhamiaji, Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) na Jeshi la Polisi, na kusisitiza kuendelezwa kwa ushirikiano huo.

Kwa upande wake, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene, ameonesha kuridhishwa na mchango na ushirikiano unaotolewa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kuimarisha utendaji wa taasisi zilizo chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, ikiwemo Uhamiaji, NIDA na Polisi.

Habari Zifananazo

2 Comments

  1. l Get paid over $110 per hour working from home. l never thought I’d be able to do it but my buddy makes over $21269 a month doing this and she convinced me to try. The possibility with this is endless….

    This is what I do………………………………….. https://Www.Cash54.Com

  2. Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
    .
    M­­­­­­o­­­­­­r­­­­­­e­ D­­­­­­e­­­­­­t­­­­­­a­­­­­­i­­­­­­l­­­­­­s For Us→→→→→→→→→→ https://Www.Payathome9.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button