SMZ: Miradi Itekelezwe Kwa Viwango

MAKAMU wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Hemed Suleiman Abdulla, amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itahakikisha miradi yote ya maendeleo, hususan miradi ya kimkakati, inatekelezwa kwa viwango vinavyokubalika.
Katika sherehe za maadhimisho ya miaka 62 ya Mapinduzi, miradi 110 ilifunguliwa na kuwekwa mawe ya msingi Unguja na Pemba, ikiwa ni pamoja na barabara, shule, viwanja vya michezo, maji safi na salama, na miradi ya kukuza biashara na uchumi. SOMA: Kasi ya maendeleo Zanzibar uhalisia Mapinduzi ya 1964

Hemed pia amebainisha kuwa uchumi unaendelea kukua na huduma za jamii zimeimarishwa, huku serikali ikijipanga kuhakikisha upatikanaji wa umeme wa uhakika Visiwani Zanzibar, jambo linalotarajiwa kuongeza uwekezaji na pato la Taifa. Pia amesema serikali itaendelea kuendeleza ujenzi wa Uwanja wa Zanzibar Arena Fumba kwa ajili ya michuano ya AFCON 2027.



