Snura aacha muziki

DAR-ES-SALAAM: MWIMBAJI wa muziki wa mduara nchini, Snura Mushi ametangaza kuacha muziki kuvitaka vyombo vya habari na wote wenye nyimbo zake kuacha kuzipiga popote.

Akizungumza leo Julai 29, 2024 Snura amesema amefikia uamuzi huo lengo kujikita kwenye dini kwa kumrudia Mungu.

“Nisiwe muongo najutia sana niliyoyafanya na maamuzi yangu, niliyafanya miaka miwili iliyopita na nina miaka miwili sijafanya sanaa”,amesema Snura

Advertisement

Aliongezea “Mwanzoni wazo langu lilikuwa kuacha kimya kimya nisiseme kwa yoyote lakini nikaona ipo haja ya kuzungumza,” amesema Snura.

SOMA:  Sitegemei muziki kuendesha maisha- Young Killer

Amesema ameamua kuweka wazi kwa sababu hataki kuwa sababu ya vizazi vijavyo kuharibika kupitia nyimbo zake.

“Na ndio maana nikaona kuna sehemu naweza kusimamisha hivyo vitu hasa upande wa vyombo vya habari, najua ni watu waelewa san asana, nisingeweza kupita kila redio na Tv natumia fursa hii kwa heshima kufikisha hili,” ameongeza Snura.