Sitegemei muziki kuendesha maisha- Young Killer

RAPA anayefanya vizuri kwenye muziki wa Hip hop nchini, Erick Msodoki ‘Young Killer’ amesema anafanya muziki kama kujifurahisha na siyo kazi, ambayo anaitegemea kuendesha maisha yake.

Akizungumza na gazeti hili msanii huyo amesema hicho ndio kinacho mtofautisha na wanamuziki wengi wa Tanzania.

“Kazi ya muziki kwangu ni kufurahi na marafiki na mashabiki zangu na sitoi macho kama kazi inayoendesha maisha yangu, ndio maana ngoma zangu zinapishana muda mrefu tofauti na ilivyo kwa wasanii wengine ambao hutoa ngoma hapa kwa hapa,” amesema Young Killer.

Msanii huyo amesema anajivunia umaarufu aliokuwa nao ambao umetokana na muziki huo lakini siri ya jina lake kuwa kubwa ni kufanya muziki wa peke yake usiofanana na rapa yeyote nchini.

Kuhusu maendelezo ya muziki wa hip hop alisema kulinganisha na ilivyokuwa zamani hivi sasa muziki huo una mashabiki wengi na hiyo
nikutokana na wasanii wengi kufanya kazi nzuri zinazo wavutia wasikilizajį.

Young Killer anayemiliki albamu itwayo TMA Swahili Rapa amewahi kutamba na wimbo wake wa Dear Gambe ambao ulifanya vizuri na kumpatia mashabiki lukuki.

Habari Zifananazo

Back to top button