“Soko lipo miundombinu umeme”
SERIKALI imekiambia kiwanda cha kuzalisha nyaya za umeme pamoja na transfoma cha Elsewedy kuwa soko lipo la kutosha nchini, na nje ya nchi na wanaendelea kuwatafutia masoko makubwa, kama ya Jumuiya ya Afrika Mashariki EAC na kwingine.
Imekitaka kuhakikisha inapeleka bidhaa zake katika masoko ya nchi za EAC, Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) na hata katika eneo huru la Biashara Afrika (AfCFTA) ili kukuza uchumi wa nchi.
Amesa tayari kiwanda hicho kimekuwa kikipeleka bidhaa hizo kwa nchi tatu tu za Afrika Mashariki ambazo niKenya, Rwanda na Burundi.
Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk Ashatu Kijaji amesema hayo leo Dar es Salaam alipofanya ziara katika kiwanda hicho kilichoko eneo la Kisarawe 11, Kigamboni Dar es Salaam.
Amesema kiwanda hicho kilifunguliwa na Rais Samia Suluhu Hassan akiwa na kazi ya kufungua mipaka ya taifa ili kupata wawekezaji wazuri wa kuja kuwekeza na bidhaa zinazozalishwa ni zenye viwango vya kimataifa.
“Kiwanda hiki kinazalisha bidhaa mahsusi kwa ajili ya kwenda nchi za Kenya, Rwanda, Afrika Kusini na hata Demokrasia ya Kongo jambo ambalo lina mafanikio makubwa kwa Watanzania,” amesema Kijaji na kuongeza kuwa ni kiwanda kilichoajiri vijana wa kitanzania zaidi ya 200.
“Mmeanza kwa nchi tatu tuu bado kuna ziada, ukifika Burundi wanaendelea kujenga sana nchi yao, tushirikiane tufikie hata soko la Uganda tupeleke bidhaa zetu kwa pamoja,” amesema Kijaji.
Amesema atatuma timu ya waofisa wake katika kiwanda hicho inayohusika na biashara ya nje kwenye Wizara ili kwa pamoja wakae waongee ili kuangalia na kuchambua bidhaa hizo kama ziko kwenye orodha ya kuingia katika nchi zote 54 za Afrika zipelekwe kwa kuwa zinazalishwa hapa nchini.
Aidha amesema Rais Samia amefanya kazi kubwa ya kuondoa vipingamizi vya biashara kwa kiwango kikubwa na vilivyobakia ni vichache sana na kwamba serikali iko tayari kuendelea kuvifanyia kazi ili kufanya kazi kwa urahisi.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Elsewedy kwa EAC,Ibrahim Qamar amesema kiwanda hicho kilianzishwa ili kuifanya Tanznaia kuwa kitovu cha uzalishaji wa bidhaa hizo kwa afrika mashariki na Afrika kwa ujuml alakini pia hata kupenya katika masoko mbalimbali duniani.
Mtaalamu wa Logistiki kiwandani hapo Ishaka Ridhwan amesema wamefanikiwa kufikisha bidhaa katika nchi za Kenya, Rwanda Burundi na tayari kwa Kenya wamepeleka zaidi bidhaa za gharama ya dola za Kimarekani 10,000 kwa mwaka jana.