Spika atoa maelekezo uwekezaji bandarini

DODOMA; SPIKA wa Bunge Dk. Tulia Ackson amewataka wabunge kuendelea kusikiliza maoni mbalimbali yanayotolewa na wananchi kuhusua suala la uwekezaji bandarini, lakini upande wao kuzungumza bungeni ulishapita na Bunge tayari lilimaliza kazi yake.

Hata hivyo amesema kwa vile kazi ya bunge ni kuishauri na kuisimamia serikali, inaweza kufanya hivyo pale serikali itakapoleta hoja zake bungeni kuhusu suala la mikataba itakayoingia.

Kutokana na hali hiyo, Dk Tulia amewataka wananchi wasihofu, kwani kazi ya Bunge ni kuishauri na kuisimamia serikali, hivyo ikiletwa bungeni hoja kuhusu mikataba wanayoingia, Bunge litafanyia kazi na kuishauri serikali.

Habari Zifananazo

Back to top button