Stars wapo kamili kuiua Uganda

KOCHA Msaidizi wa timu ya soka ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’, Hemed Suleiman ‘Morocco’, amesema wamejianda kushinda mchezo wa marudiano wa kuwania kufuzu fainali za Afcon dhidi ya Uganda ‘The Cranes’ Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam kesho.

Akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari, kocha huyo ameeleza kuwa wamewaanda wachezaji wao kimbinu na kisaikolojia kuhakikisha wanapata matokeo mazuri na kuendelea kujiweka katika mazingira mazuri ya kufuzu fainali hizo.

“Wachezaji wetu wote wapo katika hali nzuri na kila mmoja anatambua umuhimu wa ushindi, ingawa tunajua mchezo utakuwa mgumu kwa sababu Uganda watakuja kwa nguvu, lakini tumejipanga kuhakikisha tunawadhibiti na kushinda mchezo huo,” amesema Morocco.

Katika mchezo wa kwanza uliochezwa Misri Ijumaa iliyopita Tanzania iliibuka na ushindi wa bao 1-0.

Habari Zifananazo

Back to top button