Steve awalipua wasiojitokeza msibani

MSANII wa Bongo Movie Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ amewajia juu wasanii wa Bongo Fleva wenye taboa ya kutofika msibani na kudai hawataki umoja.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam wakati wa mazishi ya msanii wa Bongo Movie Grace Mapunda Steve amesema wasanii wa bongo ukienda msibani ustaa haupungui.

“Yaani wanaona wakija msibani umaarufu wao kama utashuka wakati hili ni jambo la kijamii na tasnia moja tunategemeana lakini wao wanajiona ni ujinga wanachofanya sio kujiona Michael Jackson.

Advertisement

“Wao pia nibinadamu kila nafasi itaonja mauti sio kitu kizuri kutoshiriki katika misiba wangefika hata nyumbani au kuja tu kuaga halafu waondoke,”amesema Steve

Pia ameongeza kwa kumpongeza Rajab Abdul ‘Harmonize’ kwa kujitokeza na kuwafariji wanafamilia nyumbani huo ndo ungwana unaotakiwa